Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 06, 2022 Local time: 09:21

Tatizo la uchumi, rushwa vimepunguza kura za ANC Afrika Kusini


Rais Cyril Ramaphosa

CHAMA tawala cha African National Congress (ANC) nchini Afrika Kusini kimerejea madarakani, kwa kura asilimia ndogo ikilinganishwa na chaguzi zilizopita.

Vyanzo vya habari nchini humo ANC, imeongoza kwa kupata asilimia 58 ya kura zote na kufuatiwa na Chama cha Democratic Alliance (DA) kilichopata asilimia 21, wakati chama kilichochukuwa nafasi ya tatu ni cha Economic Freedom Fighters (EFF), ambacho kimejipatia kura asilimia 11.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC kudororo kwa uchumi na rushwa ndivyo vilivyoshusha umaarufu wa chama hicho kikongwe cha ANC.

Baada ya kutangazwa matokeo kiongozi wa ANC, Cyril Ramaphosa,aliwataka wananchi kuungana na kujenga Afrika Kusini yenye umoja.

Alisema kuwa ushindi huo umeonyesha kuwa wananchi wa taifa hilo bado wanaimani na ANC tangu ilipoingia madarakani mwaka 1994.

β€œNa sasa tufanye kazi kwa pamoja, watu weusi, wazungu wanaume kwa wanawake, vijana na wazee kujenga Afrika Kusini yenye umoja ni jukumu letu sote, ” Rais Ramaphosa aliwaambia wafuasi wake mjini Pretoria.

Alisema kwamba anaitaka Afrika Kusini ambayo sio ya kiubaguzi wa rangi, kijinsia,kidemokrasia na kimafanikio.

Taarifa zaidi zinasema kuwa chama hicho kimepata asilimia 65 katika mabunge yote mawili idadi ambayo imeporomoka ikilinganishwa na asilimia 73 ilizopata miaka mitano nyuma.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG