Miaka takribani mitano tangu kuwepo serikali za ugatuzi nchini kenya ilitathminiwa kuwa imeonekana kuwepo na hatua zote za mafanikio na mapungufu ndani ya kaunti 47 zilizo chini ya utawala wa Rais Uhuru Kenyatta.
Wakili Allan Nyange wa Mombasa nchini kenya aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba mambo ya wazi wazi yaliyoonekana kuleta mafanikio ni kwa mara ya kwanza kuna uhusishaji wa karibu wa mwananchi katika masuala ya utawala na uongozi bora.
Mahojiano ya wakili Allan Nyange na VOA.
Bwana Nyange alisema kwamba ule utaratibu wa kutengeneza bajeti ambapo kwa sasa hivi serikali za ugatuzi huwa zina vikao vya kujadili bajeti na wananchi kabla bajeti hiyo haijapelekwa katika bunge la kaunti kupitishwa na wajumbe katika hizo gatuzi 47.
Kwa upande mwingine wakili Nyange alizungumzia mambo muhimu ya kufanyika ili kuweza kuondoa utata uliopo katika baadhi ya sekta ambazo zinaonekana kutofanya vyema katika serikali ya ugatuzi. Alisema washika dau ambao ni serikali kuu na serikali za kaunti ni vyema wakae pamoja ili kujaribu kulainisha hasa suala la mishahara na suala la kupandisha wahudumu vyeo.
Pia alizungumzia mambo mengine kama ufisadi jambo ambalo kwa upande wake alisema “ni vigumu sana kujaribu kulainisha hilo tatizo lakini nimeona tume ya kupambana na ufisadi wameamua watafungua ofisi katika gatuzi zote 47” ili waweze pia kupambana na ufisadi katika kaunti zote kama njia mojawapo ya kutatua tatizo.