Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 08:41

Tanzania yatuma wataalam wa afya kuchunguza ugonjwa ambao umeua watu 5 kaskazini mwa nchi


Carte de la Tanzanie
Carte de la Tanzanie

Serikali ya Tanzania imesema kwamba imetuma timu ya wataalam wa afya kuchunguza ugonjwa usiojulikana ambao umeua watu watano.

Ugonjwa huo uligunduliwa miongoni mwa watu saba wenye dalili ikiwemo homa, kutapika, kutokwa na damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili na tatizo la figo, wizara ya afya ilisema katika taarifa jana Alhamisi.

Serikali ilituma timu ya kukabiliana kwa haraka na ugonjwa huo katika mkoa wa kaskazini magharibi wa Kagera ambao unapakana na Uganda kuchunguza ugonjwa huo wa kuambukiza, daktari mkuu wa Tanzania Tumaini Nagu amesema katika taarifa.

“Sampuli zimechukuliwa kutoka kwa wagonjwa na waliofariki katika jitihada za kubaini chanzo na aina ya ugonjwa huo,” Tumaini amesema, akiwataka wanainchi kuwa watulivu lakini wachukuwe tahadhari ili kujiepusha na maambukizi.

XS
SM
MD
LG