Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 09, 2023 Local time: 06:34

Tanzania yakanusha kuingilia kati uchaguzi Kenya


Ramani ya Kenya na Tanzania

Serikali ya Tanzania imekanusha madai ya kwamba imekuwa ikiingilia uchaguzi wa kenya unaotarajiwa kufanyika agosti nane.

Tuhuma hizo za kuingilia uchaguzi nchini Kenya zimekanushwa Jumatatu jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , kikanda na kimataifa Dkt Augustine Mahiga.

“Hatujawahi kuingiliana, Kenya haijawahi kuingilia Tanzania na Tanzania haijawahi kuingilia Kenya, leo kwa nini iwe hivyo?”

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, Waziri Mahiga katika mkutano na waandishi, alikuwa na lengo la kuzungumzia pia vikwazo vya kibiashara baina ya Tanzania na Kenya vilivyoibuka hivi karibuni.

“Sisi tunautaratibu wetu wa Afrika Mashariki tunatembeleana, na tunafanya kazi pamoja,” amesema.

Mahiga amesema hawa wanaosambaza taarifa hizi kwenye vyombo vya habari au ambao wanazungumza bungeni wanalo lao jambo.

“Tuwe macho inawezekana hata watu wa nje wanaingilia kujaribu kutugombanisha… lakini nachukua nafasi hii tena kwa niaba ya serikali na rais wangu kuwahakikishia watu wa Kenya, serikali ya Kenya, vyombo vya habari hatuingilii uchaguzi wa Kenya,” alisema.

please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:00:43 0:00

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG