Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 14:55

Tanzania yaadhimisha siku ya Kifua Kikuu Duniani


Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwa na waziri wa afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu katika maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani.
Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiwa na waziri wa afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu katika maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani.

Wataalamu wa afya wameitaka serikali ya Tanzania iangalie upya suala la kugharamia huduma za afya hasa kwa wagonjwa wa magonjwa ya kuambukiza kama wagonjwa wa kifua kikuu. yamesemwa hayo katika siku ya maadhimisho ya Kifua Kikuu Duniani.

Wataalamu wa afya wameitaka serikali ya Tanzania iangalie upya suala la kugharamia huduma za afya hasa kwa wagonjwa wa magonjwa ya kuambukiza kama wagonjwa wa kifua kikuu. yamesemwa hayo katika siku ya maadhimisho ya Kifua Kikuu Duniani.

Pamoja na kuanzishwa utaratibu maalumu wa uchunguzi na kutoa elimu kwenye maeneo yenye hatari zaidi ya maambukizi ya ugojwa huo.

Takwimu zinaonyesha Mwaka 2022 Tanzania inakadiriwa na Shirika la Afya Duniani WHO kuwa na wagonjwa wapya wakifua kikuu takribani 132,000 na kati yao watu 25,800 hufariki dunia kwa ugonjwa huo ikiwa ni sawa na vifo 71 kwa siku vinavyo sababishwa na huduma duni kwa ngazi ya zahanati hasa maeneo ya vijijini huku wagonjwa wengi zaidi ya asilimia 45 wa kifua kikuu na familia zao wameingia kwenye umaskini kutokana na gharama za usafiri na lishe.

Mtafiti wa mambo ya afya Dkt. Elizabert Sanga amesema wananchi wengi walio vijijini wanakumbana na tatizo la kushidwa kugharamia matibabu na hata wanao lipia bima ya afya iliyoboreshwa ICHF wanashidwa kupatiwa matibabu na vipimo suala ambalo serikali inatakiwa kulitazama upya ili kuwapunguzia muda wanao tumia kutafuta matibabu badala ya kufanya shughuli za uzalishaji.

Baadhi ya viongozi walio hudhuria katika siku ya kifua kikuu duniani kitaifa Tanzania imefanyika katika wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.
Baadhi ya viongozi walio hudhuria katika siku ya kifua kikuu duniani kitaifa Tanzania imefanyika katika wilaya ya Bariadi, mkoani Simiyu.

‘‘Hata wale wananchi wanao weza kugharamia bima ya ICHF wana gharamia hiyo bima bila ya kupata matibabu au vipimo ambavyo wanavihitaji kwahiyo hapo kuna tatizo la ugharamiaji huduma za afya kwa wagojwa ambao wana magonjwa ya kuambukiza kama kifua kikuu na UKIMWI’ ameongezea Dkt Sanga

Ama kukosekana kwa fedha za kugharamia vikundi vya jamii vinavyoundwa na watu waliowahi kupata ugonjwa wa kifua kikuu inazidi kurudisha nyuma juhudi za kuwaibua wagonjwa wapya, huku kwenye jamii idadi ya wanaojitolea kuibua wagonjwa na kuwapa motisha ya kupima na kutibiwa mapema imezidi kupungua.

Daktari Rajabu Bakari akizungumza na sauti ya Amerika amesema serikali ianzishe utaratibu maalumu wa uchunguzi na kutoa elimu kwenye maeneo yenye hatari zaidi ya maambukizi ya kifua kikuu na kuhakikisha mipango miji inazingatia vigezo vya kimataifa vya kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.

Wananchi waliojitokeza katika siku ya Kifua Kikuu duniani nchini Tanzania.
Wananchi waliojitokeza katika siku ya Kifua Kikuu duniani nchini Tanzania.

‘‘Naishauri serikali iongeze juhudi katika kupambana na tatizo la ugojwa wa kifua kikuu kwa kuongeza wigo wa kuwafikia wananchi hasa kufika katika yale maeneo ambayo yana mikusanyiko mikubwa ya watu na ikiwezekana serikali pia ifanye mtaa kwa mtaa nyumba kwa nyumba ili kuweza kukabiliana na maambukizi mapya ya ugojwa wa kifua kikuu’’amesema Dkt Bakari

Hata hivyo waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kasim Majaliwa wakati wa maadhimisho ya kitaifa mkoani Simiyu amesema Kifua Kikuu ni ugonjwa mtambuka ambao sekta ya afya pekee haitoshi kutokomeza, hivyo hakuna budi kuweka mkakati wa kitaifa utakaowezesha ushiriki wa sekta nyingine katika kutokomeza Kifua Kikuu ifikapo mwaka 2030.

Suala ambalo Dkt. Elizabert Sanga anaitaka serikali izingatie huduma za afya kwenye ngazi za zahanati na vituo vya afya ikiwa pamoja na kupeleka vifaa vya kisasa vya kupimia kifua kikuu kwenye vituo vya kutoa huduma za uchunguzi na tiba ya kifua kikuu na kuongeza wafanyakazi wa afya waliopata mafunzo ili kuwezesha wagonjwa kupata vipimo vya kifua kikuu mapema.

XS
SM
MD
LG