Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:24

Tanzania yaadhimisha miaka 50 ya Uhuru


Mwalimu Nyerere akibebwa kusherehekea uhuru wa Tanzania Bara
Mwalimu Nyerere akibebwa kusherehekea uhuru wa Tanzania Bara

Kwa mwaka mzima sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara zimekuwa zikifanyika na kumalizika Ijumaa tarehe 9 Disemba 2011.

Uhuru ulipoiingia Disemba 9 mwaka 1961 Tanzania Bara au Tanganyika wakati ule, ilikuwa nchi ambayo imetewaliwa na wakoloni wa kijerumani na waingereza kwa miaka 43. ilikuwa nchini ndogo iliyokabiliwa na wakati mgumu kuleta maendeleo kwa sababu wakoloni hawakushughulika sana na kuleta maendeleo nchini humo.

Uzito wa kazi hiyo ulijionyesha katika kauli za mwanzo mwanzo za mtu aliyeongoza juhudi za kutafuta uhuru nchini humo Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

“ uhuru, uhuru, uhuru nafikiri nilisema jana ingawa ndugu zangu nasema niliapa, kwa kweli tuliapa, wote tuliapa, na nyinyi mliapa, au kama hakuapa nyinyi vile vile basi muwachie tu wawatawaleni. Lakini kama hii ni nchi ya waungwana watu walio sawa sawa, si nchiu ya mabwana na watwana na watwana lakini watu ni waungwana basi nyinyi mumeapa vile vile kwamba kila mmoja wenu atajitahidi kuifanya ile kazi yake aliyonayo kama kwamba yeye vile vile alishika msahafu akaapa mbele ya mwenyezi Mungu na mbele ya wananchi wenzake – Ndugu zangu hivyo ndivyo nina amini, kwamba wote nyinyi na mimi sote tumeapa kwamba Tanganyika ile tuliyopokea si Tanganyika ambayo kweli tunaweza kwa fahari na majivuno tukawaridhisha watoto wetu, kwamba tumeapa kuwatengenezea Tanganyika bora zaidi. ”

Kipindi cha utawala wa Mwalimu Nyerere kilikuwa na umuhimu wa kipekee katika kujenga utaifa na mwelekeo wa nchi hiyo changa na haikuchukua muda mrefu mara baada ya mapinduzi ya visiwa vya Zanzibar kwa pande hizo mbili kuunda muungano mwaka 1964 ndipo ikazaliwa jamhuri ya muungano ya Tanzania.

Charles bwenge ni professa katika chuo kikuu cha Florida nchini Marekani. Anaelezea kazi ya kwanza iliyokabili nchi hiyo katika miaka ya mwanzo ya uhuru na baada ya muungano na Zanzibar.

“utakumbuka hiyo miaka ya ’60 nchi nyingi sana za Afrika zilizokuwa makoloni ndio kipindi ambacho kiasi kikubwa nchi za Afrika zilipata uhuru. Na ninafikiri kazi kubwa iliyokuwepo katika miaka ya mwanzo ya uhuru ni kujenga na kuimarisha utaifa.”

Lakini kwa hakika hatua kubwa kwa Tanzania ilikuwa ni pale lilipotangazwa azimio la Arusha – Februari 1967 – likielezea azma ya wapi Tanzania itaelekea. Ilikuwa ni kauli thabiti na ya kipekee kwa nchi ya kiafrika kuamua kufuata sera za kujitegemea. Mwasisi wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.

“Nchi tunayokusudia kuijenga ni nchi ambayo watu wote ni sawa, nchi ya ujamaa wa kweli kweli ni nchi ambako watu wote ni sawa. Hawakugawanya katika mafungu mawili, fungu moja la mabwana na fungu la pili la watwana.Hakuna.”

Chini ya uongozi wa Mwalimu Tanzania ilikuwa kiongozi katika nchi za msitari wa mbele kupigania ukombozi wa nchi nyingine za Afrika – hasa kusini mwa Afrika kama vile Msumbiji, Afrika Kusini, Angola, Namibia, kiasi ya kwamba Tanzania ilijikuta ikigombana mara kwa mara na nchi za magharibi. Kama vile ilivyokuwa wakati wa uhuru wa Zimbabwe.

“Mana ni kweli kabisa rafiki zangu hawakutaka Mugabe ashinde au Patriotic Front washinde, hawakutaka. Na vitendo vya gavana vikatutia mashaka sana kwamba hawa wanaweza kabisa wakavuruga ushindi.”

Lakini licha ya kugombana na nchi za magharibi Mwalimu alionyesha heshima kubwa kwa nchi hizo kama vile ambavyo nchi hizo zilikuwa zikimuheshimu yeye, na hivyo hakusita kusifu nchi za magharibi pale alipoona ilikuwa ni haki kuwasifu.

“Rafiki zangu waingereza wakakubali jambo ambalo hawakulipenda….sasa huo si uungwana huo”

Mwalimu Julius nyerere aliwachia madaraka mwaka 1985 – hatua ambayo pia ilikuwa ya kipekee na kijasiri kwa barani Afrika, kiongozi kuamua kuwachia madaraka. Rais wa pili wa Jamhuri ya mwuungano wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi aliingia madarakani na kuikuta nchi ikiwa katika hali mbaya ya uchumi.

Professa Bwenge wa chuo kikuu cha Florida anasema Mwinyi alikuwa daraja katika kipindi cha mpito kutoka uchumi wa kijamaa na uchumu huria.

Utawala wa Mwinyi ulifuatiwa na awamu ya nne ya rais Benjamin mkapa. Katika kipindi hicho Tanzania ilijipatia sifa nyingine ya nadra kwa barani afrika – kuwa na marais wawili wastaafu walio hao na ambao waliondoka madarakani kwa kanuni za katiba ya nchi.

Mwalimu Nyerere (kabla ya kufariki mwaka 1999), na mzee Mwinyi waliishi katika ustaafu chini ya utawala wa rais Benjamin mkapa bila kuingilia utawala huo.

XS
SM
MD
LG