Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 06, 2023 Local time: 03:28

Tanzania yaonya wanaoitumia kupitisha dawa za kulevya


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Tanzania imesema haitakubali nchi yake kufanywa lango la kupitishia dawa za kulevya kwenda nchi za nje.

Kwa hivyo serikali imeagiza ulinzi uimarishwe katika mipaka yote.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuna tabia ya baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu kutumia Tanzania kama njia ya kupitisha dawa za kulevya kwa ajili ya kupeleka nchi za Afrika Kusini, Malawi na Zambia.

Alitoa kauli hiyo Jumamosi alipozungumza na watumishi wa kituo cha forodha cha Kasumulu kilichopo mpaka wa Tanzania na Malawi wilayani Kyela.

Waziri Mkuu alisema ili kuhakikisha jambo hilo linadhibitiwa ni vema ukaguzi wa watu wanaopita kwenye maeneo hayo pamoja na mizigo ukaimarishwa.

Alisema ni vema yakawepo maduka ya kubadilishia fedha katika maeneo hayo ili kudhibiti biashara hiyo ambayo kwa sasa inafanywa kimagendo huku Serikali ikikosa kodi.

“Biashara za magendo zidhibitiwe katika maeneo haya na yaanzishwe maduka ya kubadilishia fedha ili biashara hiyo ifanyike kihalali. Pia imarisheni vyanzo vya mapato,” alisema.

Pia Waziri Mkuu aliwataka Maofisa wa Uhamiaji katika mikoa hiyo ya mipakani kuhakikisha wanadhibiti uingiaji holela wa raia wa kigeni kwa lengo la kuimarisha ulinzi nchini.

Waziri Mkuu alisema katika baadhi ya maeneo kwa sasa zimeanza kuonekana silaha ambazo hapo awali hazikuwepo na ndizo zinazosadikiwa kutumika katika matukio ya kihalifu.

Magwaza alisema katika doria zilizofanywa mwaka 2016/17 jumla ya wahamiaji haramu 87 walikamatwa na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria. Alisema wahamiaji hao walitokea nchi za Malawi (30), Ethiopia (47), Burundi (6) Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) (4), ambapo baadhi walirudishwa makwao na wengine walifungwa katika gereza la mkoa wa Mbeya.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG