Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 12:21

Maafisa wapya Tanzania wasaini azimio la maadili


Rais John Magufuli wa Tanzania

Na Peter Clottey

Makatibu wakuu wapya wa wizara katika serikali ya Rais John Magufuli wametia saini azimio la maadili katika juhudi za kuhakikisha serikali inapambana na rushwa na kuleta uwajibikaji miongoni mwa wafanyakazi wa umma, kulingana na msemaji wa serikali Assah Mwambene.

Mwambene alisema katika mahojiano na VOA kuwa makatibu hao wapya walitakiwa kusoma azimio hilo mbele ya Rais Magufuli katika sherehe za kuapishwa kwao mjini Dar es salaam.

Kulingana na Mwambene Rais Magufuli aliwaambia makatibu wakuu hao, "kama kuna yeyote ambaye anaona hawezi kufanya kazi chini ya azimio hili la maadili, ajiondoe sasa hivi na kutoka katika viwanja vya Ikulu....Inawezekana kuna baadhi yenu mnakejeli azimio hili. Kwa hiyo, kaa kando ili tujue nani ambao hawakubaliani na azimio hili."

Hii ni mara ya kwanza kwa maafisa wapya wa serikali kutia saini azimio hilo hadharani.

Maafisa wapya kwa kawaida wanatia saini azimio ambalo baadaye huwasilishwa katika tume ya maadili. Lakini, safari hii Rais Magufuli alitaka azimio hilo liboreshwe kuingiza hatua kali za kupambana na rushwa, alisema Mwambene.

XS
SM
MD
LG