Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 31, 2023 Local time: 13:13

Maandamano ya CHADEMA yapingwa na mkuu wa sheria


Wafuasi wa CHADEMA wakati wa kampeni zilizopita.

Mwanasheria mkuu wa Serikali yaTanzania George Masaju amepinga mpango wa maandamano yanayotarajiwa kufanywa Septemba mosi na chama cha Demokrasia na Maendeleo .

Mwanasheria mkuu wa Serikali yaTanzania George Masaju amepinga mpango wa maandamano yanayotarajiwa kufanywa Septemba mosi na chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA na amekiomba chama hicho cha upinzani kutii mamlaka za dola.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es salaam Jumatatu kuhusiana na zuio la mikutano na maandamano ya vyama vya siasa, mwanasheria huyo alivitaka vyama vya siasa nchini pamoja na wafuasi wake kuwa watiifu kwa mamlaka za nchi pamoja na vyombo vya maamuzi, ili kudumisha amani na umoja wa taifa.

XS
SM
MD
LG