Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:23

Tanzania na Rwanda kuimarisha uhusiano wake.


Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) akisalimiana na rais wa Tanzania Jonh Magufuli( kulia)
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) akisalimiana na rais wa Tanzania Jonh Magufuli( kulia)

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga amesema rais wa Rwanda Paul Kagame alikuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kumpongeza rais Magufuli muda mfupi baada ya tume ya uchaguzi nchini Tanzania kumtangaza kuwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana.

Ukurasa mpya wa mahusino moto umefunguliwa baina ya Serikali za Tanzania na Rwanda baada ya rais wa Tanzania John Pombe Mgufuli kuhudhuria maadhimisho ya 22 ya kuwakumbuka watu waliokufa katika mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Augustine Mahiga amesema rais wa Rwanda Paul Kagame alikuwa kiongozi wa kwanza wa Afrika kumpongeza rais Magufuli muda mfupi baada ya tume ya uchaguzi nchini Tanzania kumtangaza kuwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika mwaka jana . Kagame pia alihudhuria sherehe za kuapishwa rais Magufuli.

Mahiga amesema utawala wa Tanzania na rwanda ulikuwa katika hali ya mvutano tangu Kagame na rais wa zamani wa Tanzania Jakaya Kikwete kushindwa kukubaliana katika masuala kadhaa. Hili lilitokea baada ya Kikwete kuisihi Rwanda kufanya mazungumzo na kundi la waasi wa kihutu la FDLR lililoko jamhuri ya kidemokrasia ya congo ili liweze kuacha kufanya harakati zake za uasi DRC.

Lakini Mahiga amesema rais Magufuli alitembelea Rwanda katika kuboresha hatua mpya za mahusiano baina ya nchi hizo mbili majirani. Pia amesema mahusiano ya pande mbili yanaweza kurahisisha biashara katika mipaka ya nchi. Tanzania hivi sasa ndio inashikilia uenyekiti wa jumuiya ya afrika ya mashariki .

XS
SM
MD
LG