Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 10:00

Meya wa Mwanza ashikiliwa na polisi


Mandhari ya mji wa Mwanza, Ziwa Victoria.
Mandhari ya mji wa Mwanza, Ziwa Victoria.

Mamlaka za serikali nchini Tanzania zimethibitisha kukamatwa kwa mstahiki meya wa jiji la Mwanza, kaskazini-magharibi mwa mji huo, Leonard Bandiho Bihondo mwenye umri wa miaka 64 kwa kuhusishwa na mauaji.

Mamlaka za serikali nchini Tanzania zimethibitisha kukamatwa kwa mstahiki meya wa jiji la Mwanza, kaskazini-magharibi mwa mji huo, Leonard Bandiho Bihondo mwenye umri wa miaka 64 kwa kuhusishwa na mauaji.

Ramani ya Tanzania.
Ramani ya Tanzania.

Bihondo amekamatwa Jumatano jioni katika uwanja wa ndege wa Mwanza akitokea jijini Dar es Salaam kwa shughuli za kikazi. Ambapo amehudumu nafasi hiyo kwa miaka 10.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi kiongozi huyo anahusishwa na maujai ya kiongozi wa CCM, kata ya Isamilo, Bahati Steven, aliyeuwawa kwa kuchomwa kisu kifuani akiwa ofisini kwake Ijumaa iliyopita.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Simon Silo amesema upelelezi huo wa mauaji ya katibu kata wa chama cha CCM bado unaendelea. Ambapo polisi waliwahoji washukiwa watatu, wote wamekuwa wanamtaja Bandiho kuwa amehusika katika tukio na kama polisi ikithibitisha bila mashaka kwamba amehusika katika mauaji haya basi atafikishwa mahakamani na kuhakikisha kwamba sheria inachukua mkondo wake.

Kuuwawa kwa kiongozi huyo wa CCM kumekuwa kukihusishwa na masuala ya kisiasa hususan uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. Mauaji hayo ambayo yamelitikisa jiji la mwanza yalielezewa na Waziri wa Mambo ya ndani Laurence Masha kuwa ni ya kinyama na yalitokea saa chache kabla waziri Masha kukutana na kiongozi huyo wa CCM na kuahidi kuwa serikali itafanya kila iwezalo kuwatia mbaroni wauaji.


XS
SM
MD
LG