Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 13:48

Tanzania imepoteza mabilioni ya fedha –Lipumba.


Mwanasiasa maarufu nchini Tanzania, Ibrahim Lipumba, anadai kuwa nchi hiyo iko katika mwelekeo mbaya wa kuanguka kiuchumi huku ikiwa tayari imepoteza mabilioni ya fedha baada ya kusitishiwa misaada kutoka Marekani kutokana na mkwamo wa kisiasa unaoendelea visiwani Zanzibar.

please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:02:53 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Profesa Lipumba ambaye pia ni mchumi aliyebobea alisema hayo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Daressalaam kuelezea hali ya kisiasa nchini humo baada ya uchaguzi mkuu uliopita.

Lipumba aliwahi kuwa mshauri wa rais katika serikali ya awamu ya pili Tanzania, amesema kuwa nchi hiyo huenda ikajikuta ikitumbukia kwenye mkondo wa mbaya iwapo itashindwa kutafutia ufumbuzi mzozo wa kisiasa unaoendelea visiwani humo.

Vijana wakiandamana Zanzibar baada ya uchaguzi
Vijana wakiandamana Zanzibar baada ya uchaguzi

Hii ni mara ya pili kwa vigogo wa kisiasa nchini kujitokeza hadharani na kuelezea wasiwasi wao kuhusiana na hali ya mambo katika visiwa hivyo vinavyosifika kwa utalii wa kimataifa. Mara ya kwanza kufanya hivyo alikuwa mwanasheria mkuu wa zamani, Mark Bomani aliyetaka kupatikana kwa suluhu haraka iwezekanavyo kwani vinginevyo hali inaweza kuwa mbaya zaidi.

Kwa upande wa Professa Lipumba aliyekuwa mwenyekiti wa chama wananchi CUF amesema kuwa siyo vyema kuachia hali kuendelea kama ilivyo visiwani humo, kwani ishara mbaya tayari imeanza kujionyesha kwa Tanzania kunyimwa msaada wa maendeleo kutoka kwa Serikali ya Marekani.

“Bodi ya MCC ilikaa tarehe 16 ikashindwa kupitisha msaada wa pili wa Tanzania na hoja iliyofanya bodi hiyo kutopitisha msaada wa dola milioni 472.8 ni kutokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar na huu msaada ulikuwa unaenda kusaidia sekta ya umeme kuweza kuwa bora zaidi” alisema Lipumba.

Suala la mzozo wa Zanzibar tangu kufutwa kwa matokeo yake miezi miwili iliyopita limekuwa mada muhimu ya majadiliano huku pande zote yaani CCM na CUF zikiendelea kushikilia misimamo inayotofautiana.

Hivi karibuni CCM ilitoa taarifa ikisema kuwa imenza kujiandaa kwa uchaguzi mwingine wa marudio na ikawataka wanachama wake kuwa tayari kwa hali hiyo, lakini kauli hiyo ilipingwa vikali na CUF.

CUF kama ilivyo pia jumuiya za kimataifa inataka kuheshimiwa na uchaguzi uliopita na inataka tume imtangaza mshindi wa uchaguzi huo. Kutokana na kuendelea kwa hali hiyo ya sintofahamu, Profesa Lipumba ameanza kuonyesha wasiwasi wake kuhusu majaliwa ya taifa.

Pamoja na mkwamo huo kumekuwa na vikao kadhaa vinavyoendelea katika ya Maalimu Seifu aliyekutana na mpinzani wake, Rais Mohammed Shein na hivi karibuni viongozi hao kwa nyakati tofauti wamekutana na Rais John Magufuli. Hakuna taarifa zaidi kuhusu kile kinachofikiwa katika mikutano yao.

XS
SM
MD
LG