Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 03:54

Tanzania kupiga marufuku mifuko ya plastiki kuanzia Julai mosi


Miful

Tanzania iko katika mchakato wa kupiga marufuku utengenezaji, uagizaji, biashara na matumizi ya mifuko ya plastiki, ambapo utekelezaji wake utaanza Julai, 2019, ikiwa ni hatua kabambe kukabiliana na uchafuzi wa mazingira.

Tanzania, inaungana na nchi ambazo hivi karibuni zilipiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki isiyoweza kuoza inapoingia ardhini na ambayo imetajwa na umoja wa mataifa kuwa miongoni mwa changamoto kubwa za mazingira.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, Kati ya bilioni 9 ya plastiki zinazo tengenezwa kote duniani, asilimia 9 pekee ndio huweza kutumiwa tena na kutokuwa sehemu ya uchafuzi wa mazingira.

Tanzania inaungana na nchi zaidi ya 60 ambazo tayari zimetangaza kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki. Nchi nyingine ni China, Ufaransa, Kenya, Rwanda na Italia.

Kenya ndio nchi yenye sheria kali zaidi Afrika Mashariki katika kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki ambapo anayekutikana na mifuko hiyo anakabiliwa na kifungo cha miaka minne gerezani au faini ya dola 40,000.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG