Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 22:57

Tanzania, Korea Kusini zaondoa viza kwa wafanya kazi wa serikali


Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Tanzania na Korea Kusini Jumapili zilitia saini mkataba wa kuondoa zuio la viza kwa raia wa nchi hizo mbili wanaosafiri kidiplomasia na kiutumishi.

Saini hizo ziliwekwa wakati wa hafla katika Ikulu ya Dar es Salaam na waziri wa mambo ya nje wa Tanzania na naibu wa waziri wa mambo ya nje wa Korea Kusini.

Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Lee Nak-yeon, ambaye yuko ziarani nchini Tanzania, alishuhudia utiaji saini wa mkataba huo kwa niaba ya serikali ya Moon Jae In huku waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akiiwakilisha serikali ya rais John Pombe magufuli.

Viongozi hao wawili walisema hatua hiyo itaimarisha uhusiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo mawili .

Akizungumza baada ya utiaji saini huo, Majaliwa alisema mkataba huo umelenga kuimarisha uhusiano, maendeleo ya kiuchumi, kiutamaduni na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama).

Majaliwa aliongeza kuwa Serikali ya Tanzania inatarajia kutekeleza miradi mingine mitatu mikubwa ukiwamo ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi mkoani Mwanza.

Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, ujumbe wa wafanya biashara wa kutoka Korea Kusini ulklitarajiwa kukutana siku ya Jumatatu na wafanyabiashara wa Tanzania katika jitihada za kuimarisha ushirikiano wa kibiashara.

XS
SM
MD
LG