Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 28, 2023 Local time: 23:26

Upinzani wagomea matokeo ya uchaguzi Tanzania


Edward Lowassa mgombea urais wa Ukawa
Edward Lowassa mgombea urais wa Ukawa

Mgombea urais wa Tanzania kupitia muungano wa vyama vya upinzani, Ukawa, Edward Lowassa amesema leo hatambui matokeo ya uchaguzi kama yanavyotolewa na Tume ya Uchaguzi na kuitaka tume hiyo kusimamisha utoaji matokeo mara moja.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Dar es salaam Jumatano Lowassa alisema kuwa hawaridhiki na matokeo yanayotangazwa kwa sababu hayalingani na matokeo walio nayo wao. Lowassa alisema tume ya uchaguzi haina budi kuanza upya hesabu ya kura kwa kutumia teknolojia mpya.

Lowassa agomea matokeo
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:47 0:00

Mapema Jumatano, Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar - ZEC - ilitangaza kufuta uchaguzi wa Zanzibar kutokana na kile ilichosema ni uharibifu mkubwa katika utaratibu mzima.

Mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha alisema kuwa mipango itafanywa ili wananchi wa Zanzibar wapige tena kura baada ya siku tisini.

Jecha alisema kuwa wajumbe wa tume ya uchaguzi wamekuwa wakigombana ndani ya tume hiyo na pia ripoti kwamba idadi ya wapiga kura kutoka vituo vya kisiwani Pemba ilikuwa kubwa kuliko inavyoonyesha katika daftari la wapiga kura.

Mgombea wa upinzani Seif Shariff Hamad alisema mara moja kuwa hakubaliani na uamuzi wa ZEC kufuta matokeo na kuitaka tume hiyo kuendelea na utaratibu wa kuhesabu kura.

XS
SM
MD
LG