Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:48

Kazi ya kuhesabu kura yaanza Tanzania


Mtu akipiga kura katika kituo mjini Dar es Salaam, Tanzania, October 25, 2015.
Mtu akipiga kura katika kituo mjini Dar es Salaam, Tanzania, October 25, 2015.

Kazi ya kuhesabu kura imeanza nchini Tanzania baada ya siku nzima ya upigaji kura Jumapili. Mamillioni ya watu kote nchini walijitokeza kupiga kura katika vituo walivyojiandikisha kuchagua marais wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar, pamoja na wabunge, wawakilishi, madiwani na masheha.

Uchaguzi Tanzania
please wait

No media source currently available

0:00 0:08:19 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva, aliambia Sauti ya Amerika katika matangazo ya moja kwa moja kuwa ana imani kuwa uchaguzi huyo utaonekana kuwa wa haki na wa wazi licha ya matatizo ya hapa na pale katika vituo.

Mpiga kura aekewa alama ya kuonyesha amepiga kura
Mpiga kura aekewa alama ya kuonyesha amepiga kura

Baadhi ya matatizo ilikuwa ni kukosekana kwa vifaa vya kupigia kura katika vituo na watu kukosa kuona majina yao katika orodha au wao wenyewe kufika katika vituo bila vitambulisho vya kupigia kura.

Hata hivyo, sehemu kubwa ya ripoti kutoka kwa waandishi wa Sauti ya Amerika katika maeneo mbali mbali nchini zimesema upigaji kura ulienda salama bila usumbufu katika vituo vingi vya upigaji kura.

Mgombea wa chama tawala CCM, John Magufuli. alipiga kura katika wilaya yake ya uchaguzi Chato katika mkoa wa Mwanza, wakati mgombea wa upinzani, Edward Lowasa, alipiga kura nyumbani kwake Monduli.

Nao wagombea urais Zanzibar, Rais wa sasa Ali Mohamed Shein wa CCM na mpinzani wake Seif Shariff Hamad wa chama cha CUF walikuwa miongoni mwa watu kwanza kujitokeza mjini Unguja kupiga kura zao.

Kulingana na tume ya uchaguzi matokeo ya kura kwa upande wa wabunge na madiwani yataanza kujulikana ifikapo usiku wa manane kwa saa za Afrika Mashariki. Matokeo ya uchaguzi wa rais yatatangazwa rasmi Oktoba 28 lakini tume imesema huenda pia yakajulikana saa 48 baada ya upigaji kura kufungwa.

XS
SM
MD
LG