Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:47

Wasanii na kampeni za uchaguzi Tanzania


Wasanii wakishirikia katika kampeni
Wasanii wakishirikia katika kampeni

Kampeni za uchaguzi mkuu nchini Tanzania mwaka huu zimepata msukumo wa aina yake kutoka kwa wasanii ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wapiga kura.

Wasanii wakiwemo wacheza filamu, wana muziki wa bongo flava na wachekeshaji wamekuwa wakisafiri na wagombea katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo na kupanda majukwaani kusisitiza umuhimu wa kushiriki zoezi la upigaji kura na kumchagua mgombea wanayempigia kampeni.

Ni dhahiri wasanii wana nafasi nafasi maalum katika uchaguzi huu, hasa pale wanamuziki wa kizazi kipya maarufu kama ‘Tukutane Januari’ walipokuwa wakipanda kwenye majukwaa kuwahamasisha vijana kushiriki kikamilifu zoezi la uandikishaji wapiga kura.

Kampeni zilipoanza baadhi ya wasanii nao wakajitokeza na ujumbe kama vile ‘Mama sema na mwanao’.

XS
SM
MD
LG