Tume ya uchaguzi nchini Tanzania imewataka wananchi kujielimisha kuhusu utaratibu na haki yao ya kupiga kura kwa njia ya amani wakati wa uchaguzi mkuu Oktoba 25.
Maafisa wa tume wanasema kwa wiki kadha sasa wamekuwa wakitoa elimu kwa wapiga kura kuhusu kile wanachotakiwa kufanya kuhakikisha hawapotezi haki yao ya kupiga kura siku hiyo itakapofika.
Watanzania wapatao millioni 22 wanatazamiwa kushiriki katika zoezi hilo. Tume ya uchaguzi pamoja na makundi ya kijamii yanatoa maelekezo kamili kwa ili wapiga kura wafanikishe zoezi hilo.
Katika mfululizo wa makala zetu maalum tunaangalia juhudi hizo za kuelimisha wapiga kura.