Vuguvugu la kampeni za uchaguzi nchini Tanzania linazidi kupamba moto. Huku ikiwa zimesalia takribani wiki mbili tayari waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa wameanza kazi yao ikiwa ni pamoja na kufanya mawasiliano na vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo utakaofanyika Oktoba 31 mwaka huu.
Ujumbe wa waangalizi kutoka Umoja wa Ulaya ulitembelea ofisi ndogo za chama tawala cha Tanzania, CCM na kufanya mazungumzo na meneja wa kampeni wa chama hicho Abdulrahmani Kinana, kuhusu mchakato wa uchaguzi mkuu.
Ujumbe huo wa watu wawili ulioongozwa na mwangalizi mkuu msaidizi wa EU, Tony Rase, ambaye alifuatana na afisa wa masuala ya siasa, jinsia na haki za binadamu Stephen Mondon.