Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 11, 2024 Local time: 16:25

Tanzania: CHADEMA kuanza tena maandamano


Mkutano wa hadhara wa chama cha CHADEMA kumaliza kampeni za uchaguzi wa 2010
Mkutano wa hadhara wa chama cha CHADEMA kumaliza kampeni za uchaguzi wa 2010

Chama cha maendeleo na demokrasia CHADEMA kimesema kitaendelea na maandamano na mikutano ya hadhara.

Chama cha maendeleo na demokrasia CHADEMA nchini Tanzania, kimesema kitaendelea na mikutano yake ya hadhara na maandamano licha ya kukosolewa na wakuu wa serikali na baadhi ya wananchi.

Baraza kuu la chama hicho limetoa maazimio kadhaa ambayo wanatarajia kuwaeleza wananchi katika mikutano yao itakayoanza tena hivi karibuni.

Freeman Mbowe mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA amesema moja ya matatizo makubwa kwa sasa hapa nchini ni tatizo kubwa la mgao wa umeme.

“ Wananchi wanateseka, wananchi wana mgao, chimbuko la msingi la mgao na tatizo la umeme katika taifa hili ni kwamba miradi ya nishati ya umeme imegeuzwa kuwa miradi ya kunufaisha wakubwa na washirika wao. Kumekuwa hakuna mkakati wa nguvu na makusudi kuhakikisha ufumbuzi huu unapatikana kwa sababu watu hawajagundua kupitia miradi ya umeme watu wanatengeneza mabilioni na mabilioni ya pesa za bure za wizi”

Katika mahojiano na mwandishi wetu George njogopa bwana Mbowe amesema chama chake kinatowa woito wa kufutwa kazi waziri wa nishati kwqa kushinda kutekeleza wajibu wake na kwamba maandamano yao ni ya amani.

“Maandamano yetu ni ya amani, matakwa katika maandamano yetu yamekuwa wazi wazi kabisa hatujawachochea wananchi kufanya vurugu mahali popote. Mikutano yetu imekuwa ya amani sana na itaendelea kuwa ya amani.”

Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, mikutano ya CHADEMA sasa itaelekea nyanda za juu kusini huku kukiwa na shinikizo kutoka Serikali na chama tawala CCM kwamba mikutano hiyo inahatarisha amani na kuchochea vurugu.

XS
SM
MD
LG