Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 07:12

Zitto ataka bunge la Tanzania kupambana na tuhuma za rushwa


Bunge la Tanzania mjini Dodoma.
Bunge la Tanzania mjini Dodoma.

Bunge la Tanzania limekanusha taarifa iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kubadilishwa kwa kamati za kudumu za bunge kutokana na tuhuma za kashfa ya rushwa dhidi ya baadhi ya wakuu wa kamati hizo.

Bunge limetoa taarifa kwenye mtandao wa Tweetter likieleza kwamba mabadiliko ya baadhi ya wajumbe wa kamati ni ya jambo la kawaida.

Taarifa hiyo imetolewa kufuatia ripoti kwenye gazeti la Mtanzania inayoeleza kwamba wabunge Zitto Kabwe wa Kigoma Mjini na Hussein Bashe wanajiuzulu kutoka nafasi zao kutoka kamati ya huduma za jamii.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:54 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akizungumza na Sauti ya Amerika Zitto Kabwe amesema amechukua hatua hiyo ili kuweka shinikizo kwa Spika wa bunge la Taifa kuweza kuchukua hatua kutokana na tuhuma hizo.

Zitto amesisitiza kwamba, kumekuwa na tabia katika bunge ya kutochukua hatua au uchunguzi kufanyika pindi kunakuwepo na tuhuma za aina yeyote dhidi ya wabunge.

XS
SM
MD
LG