Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 04, 2023 Local time: 15:33

Tani 1.8 za dawa za kulevya zakamatwa Nigeria


Magunia ya kokeini yenye uzani wa tani 5,2 na boti iliyokamatwa yanaonyeshwa kwa vyombo vya habari katika kituo cha Jeshi la Wanamaji la Ureno huko Almada, kusini mwa Lisbon, Oktoba 18, 2021.AP.

Maafisa wa usalama wa Nigeria wanasema wameweza kukamata tani 1.8 za kokeni kutoka ghala moja mjini Lagos ikiwa ni idadi kubwa kabisa kuwahi kupatikana nchini humo.

Msemaji wa Idara ya Kitaifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Nigeria alisema Jumatatu kwamba dawa hizo zinaweza kufikia thamani ya milioni 278.5 za kimarekani.

Idara hiyo ilisema dawa hizo, zilizopatikana katika ghala la makazi siku ya Jumapili, zilikusudiwa kwa wanunuzi wa Ulaya na Asia.

Afrika Magharibi ni kitovu kikuu cha kupitisha kokeini inayotengenezwa Amerika Kusini na kuuzwa Ulaya. Mwezi Aprili, polisi nchini Ivory Coast walikamata zaidi ya tani mbili za kokeini, huku maafisa katika kisiwa cha Cape Verde walikamata tani 9.5 za kokeini mwaka 2019.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu ilisema kwamba kunaswa kwa kokeini ulimwenguni kumefikia rekodi ya juu ya tani 1,424 mwaka 2020.

Idara hiyo ya Nigeria iliwakamata watu watano kutokana na msako huo ambao ilisema ni wanachama wa mtandao wa kimataifa wa dawa za kulevya ambao ulikuwa ukifuatiliwa tangu mwaka 2018 kwa kushirikiana na taasisi ya kupambana na dawa za kulevya ya Marekani.

Miongoni mwa waliokuwa kizuizini ni pamoja na Wanigeria wanne na raia mmoja wa Jamaica.

XS
SM
MD
LG