Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 21, 2024 Local time: 20:30

Adele na Beyonce : 'Chuma Hunoa Chuma'


Adele akipokea tuzo
Adele akipokea tuzo

Adele ameshinda tuzo ya trifecta- albam ya mwaka, rekodi ya mwaka na nyimbo ya mwaka- katika Tamasha la 59 la Grammy lililofanyika Los Angeles Jumapili usiku.

Lakini Adele aliuthibitishia umma uliohudhuria tamasha hilo ule usemi kwamba chuma hunoa chuma kwani mtu hufundishwa na wenzake.

Mwanamuziki huyu wa Uingereza amemshinda supasta wa muziki wa pop Beyonce kwa album 25 na nyimbo yake maarufu iliyouza sana Hello.

Lakini alipopanda kwenye jukwaa kupokea tuzo ya rekodi ya mwaka kwa nyimbo yake Hello, alimwagia sifa kemkem supasta mwenzie.

Adele azungumzia ndoto yake

“Ndoto yangu na shujaa wangu ni Queen B, na kuhusudu sana. Wewe una ukonga moyo wangu kila siku na umefanya hivyo kwa miaka 17. Nakuhusudu sana na nataka uwe mama yangu, sawa kabisa?”

Mwanamuziki Adelle amepata ushindi mkubwa wa mara tatu wa album ya mwaka, rekodi ya mwaka na nyimbo bora ya mwaka katika tuzo za 59 za Grammy jana usiku huko Los Angeles, Carlifornia na kumshinda Beyonce katika maeneo hayo matatu .

Adele amesema “ndoto yangu na mtu ambaye ni mfano kwa maisha yangu ni Queen B na nataka wewe uwe mama yangu.”

Beyonce akitumbuiza katika tamasha la Grammy
Beyonce akitumbuiza katika tamasha la Grammy

Onyesho maalum la Beyonce

Mapema katika usiku huo Beyonce alifanya onyesho maalum kwanza likionyesha picha ya video akiwa mjamzito na tumbo lake likionekana wazi wazi akiwa na watoto mapacha. Na baadaye kujitokeza yeye mwenyewe kukamilisha show yake hiyo.

Beyonce hakuondoka patupu katika tamasha hilo, kwani alishinda tuzo ya Grammy ya albam bora ya miji ya kisasa kwa nyimbo yake maarufu Lemonade. “Sote tunapitia maumivu na kupoteza, na mara nyingi tunalemewa. Nia yangu juu ya filamu na album ilikuwa kutengeneza sanaa ambayo itatoa sauti kwa maumivu yetu, mapambano yetu, kizazi chetu na historia yetu. Ilituweze kupambana na mambo yanayotukera.”

Sauti Nyororo ya Adele

Adele mwenye kusifika kwa sauti yake nyororo pia alishinda wimbo bora wa mwimbaji mmoja mmoja na pop.

Tamasha la mwaka huu la Grammy, lilikuwa na ushindani mkubwa hususan kati ya wanamuziki maarufu Beyonce na Adele.

Vifijo na Pongezi

Lilikuwa limepambwa kwa vifijo na pongezi za sifa kwa waliokuwa wakitumbuiza, kuanzia kuonekana Beyonce huku akiwa mjamzito akionyesha kilele cha kuwa mzazi, pia namna muziki wa Bruno Mars ulivyokuwa umefanana na muziki wa marehemu Prince ambaye ni gwiji wa muziki wa rock.

Washindi wengine wa Jumapili ni pamoja na Chance ambaye ameshinda tuzo tatu, ikiwemo mwanasanaa bora mpya, ambaye hakuuza muziki wowote, na mwanamuziki anayeinukia kuwa supasta Maren Morris.

Kwa hivyo tamasha hilo la Grammy limeonyesha vipaji vinavyoendelea kukuwa na jinsi wasanii walivyokuwa tayari kujifunza kutoka kwa masupasta wenzao kama tulivyoona Adele juu ya ushindi wake aliendelea kuonyesha kuwa Beyonce pia ni gwiji la muziki ambaye amemsaidia kupata ushindi huo.

XS
SM
MD
LG