Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 09, 2024 Local time: 20:51

Taliban wanataka kubadilishana wafungwa na Marekani


Wafungwa katika gereza la Guantanamo Bay, Cuba
Wafungwa katika gereza la Guantanamo Bay, Cuba

Serikali ya Taliban nchini Afghanistan imeonyesha nia ya kuawachilia wafungwa wawili raia wa Marekani kwa kubadilishana na raia wa Afghanistna wanaozuiliwa Marekani.

Msemaji mkuu wa serikali ya Taliban Zabihullah Mujahid, ameambia waandishi wa habari mjini Kabul kwamba swala la kuwaachilia huru wafungwa limejadiliwa wiki hii katika mkutano na maafisa wa Marekani mjini Doha, namna lilivyoangaziwa katika mikutano ya awali.

Mujahid amesema kwamba matakwa ya Afghanistan ni lazima yatimizwe na kwamba wana raia wake wanaozuliwa Marekani na Guantanamo.

Bila kutoa maelezo zaidi kuhusu raia wa Afghanistan wanaozuiliwa katika gereza la Marekani la Guantanamo Bay nchini Cuba, Mujahid amesema kwamba wanastahili kuwaachilia huru wafungwa kwa kubadilishana.

Forum

XS
SM
MD
LG