Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:46

Taliban wamteua balozi wao kwenye UN, wataka wapewe fursa ya kuhutubia kikao


Wataliban.
Wataliban.

Taliban wameomba kuhutubia viongozi wa dunia kwenye mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York wiki hii.

Wamemteua msemaji wao alioko Doha Suhail Shaheen kama balozi wa Afghanistan kwenye Umoja huo, kulingana na barua ambayo shirika la habari la Reuters limeiona Jumanne.

Waziri wa mambo ya nje wa Taliban Amir Khan Muttaqi amewasilisha ombi hilo katika barua iliyotumwa kwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres Jumatatu.

Muttaqi aliomba kuzungumza wakati wa kikao cha ngazi ya juu cha baraza kuu la Umoja wa mataifa ambacho kilimalizika Jumatatu.

Msemaji wa Guterres, Farhan Haq amethibitisha barua hiyo ya Muttaqi.

Haq anasema barua ya Taliban ya kutaka wapewe kiti kwenye Umoja wa mataifa ilitumwa kwa kamati ya nchi 9 wanachama, ikiwemo Marekani, China, na Russia.

XS
SM
MD
LG