Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 07:09

Taliban wamewacharaza viboko waliofanya mapenzi nje ya ndoa Afghanistan


Afisa wa usalama wa Taliban akiwa ameshika doria wakati wa watu wanaodaiwa kufanya makosa mbalimbali walipokuwa wanapigwa viboko katika mjiwa Charikar, December 8, 2022
Afisa wa usalama wa Taliban akiwa ameshika doria wakati wa watu wanaodaiwa kufanya makosa mbalimbali walipokuwa wanapigwa viboko katika mjiwa Charikar, December 8, 2022

Maafisa wa Taliban kusini mwa Afghanistan, wamewacharaza viboko watu 27 wakiwemo wanawake wawili, kwa madai ya wizi, kufanya mapenzi nje ya ndoa na makosa mengine.

Adhabu hiyo imetolewa kusini katika majimbo ya Helmand na Zabul.

Msemaji wa serikali ya jimbo Mohammad Qasim Riyaz, amesema kwamba wanaumme 20 wamecharazwa viboko hadharani katika uwanja wa michezo katika mji mkuu wa Lashkar Gah.

Kila mwanamme amepigwa viboko kati ya 35 na 39 huku idadi kubwa ya watu wakiwemo viongozi wa Taliban, viongozi wa kidini na viongozi wengine wa kieneo wakishangilia.

Baadhi ya waliopigwa viboko, walihukumiwa kifungo.

Katika tukio jingine, shirika la habri linalomilikiwa na utawala wa Taliban limeripoti kwamba wanaumme watano na wanawake wawili wamecharazwa viboko kwa kuwa katika uhusiano haramu, wizi wa kibamavu na makosa mengine huko Qalat, mji mkuu wa jimbo la Zabul.

Viongozi wenye msimamo mkali nchini Afghanistan wamekuwa wakiwatandika watu viboko katika viwanja vya michezo vilivyofurika watu, katika siku za hivi karibuni.

XS
SM
MD
LG