Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:49

Taliban wamefunga matangazo ya VOA Afghanistan


Msemaji wa utawala wa Taliban Zabihullah Mujahid akisaliana na mwandishi wa habari baada ya kuhutubia waandishi wa habari mjini Kabul Aug 17, 2021
Msemaji wa utawala wa Taliban Zabihullah Mujahid akisaliana na mwandishi wa habari baada ya kuhutubia waandishi wa habari mjini Kabul Aug 17, 2021

Serikali ya Afghanistan, inayoongozwa na kundi la wapiganaji wa kiislam la Taliban, imesema kwamba hatua yake ya kufunguza matangazo ya vyombo vya habari vya Marekani ikiwemo Sauti ya Amerika, inatokana na kwamba matangazo hayo yalikuwa yanavunja sheria za nchi hiyo.

Taliban, wamefungia matangazo ya VOA, Azadi Radio, jana alhamisi, siku moja baada ya wizara ya habari na utamaduni ya Taliban kusema kwamba ilikuwa imepokea malalamishi kuhusu maudhui yanayopeperushwa na vituo hivyo, bila kutoa mifano maalum.

Haijafahamika iwapo marufuku hiyo itatekelezwa dhidi ya mashirika mengine ya habari ya kimataifa yanayotumia mfumo wa FM kupeperusha matangazo yake nchini Afghanistan.

Katika taarifa kwa Sauti ya Amerika, VOA, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Afghanistan Abdul Qahar Balkhi, amesema kwamba Afghanistan ina sheria inayosimamia vyombo vya habari na shirika lolote linalovunja sheria hizo litafungiwa kupeperusha matangazo yake nchini humo.

Kaimu kurugenzi wa Sauti ya Amerika Yolanda Lopez amesema kwamba VOA inafanya kazi yake kwa kuzingatia sheria za uandishi wa habari bila mapendeleo yoyote na huwafikia wasikilizaji milioni 7.3 kila wiki, nchini Afghanistan.

XS
SM
MD
LG