Kundi la Taliban limesema Jumatatu kwamba vikosi vyao vya usalama vimewaua na kuwakamata wanachama kadhaa muhimu washirika wa kundi la Islamic State, kwa kupanga mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni nchini Afghanistan, wakidai kuwa washukiwa hao walivuka mpaka kutoka Pakistan.
Zabihullah Mujahid, msemaji wa Taliban aliorodhesha madai hayo na kile kinachoitwa mafanikio dhidi ya Islamic State-Khorasan, au IS-K, inayojulikana kama Daesh, katika taarifa isiyo rasmi bila kutoa ushahidi wa kuwaunga mkono.
Madai hayo yamekuja baada ya majirani watatu wa karibu wa nchi hiyo na Russia, kwa pamoja kuitaka serikali ya Kabul, hapo Ijumaa iliyopita kuchukua hatua zinazoonekana na zinazothibitishwa dhidi ya makundi ya kigaidi ya kimataifa, ikijumuisha IS-K, katika ardhi ya Afghanistan.
Forum