Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 09, 2023 Local time: 10:25

Waasi walenga ofisi za NATO nchini Afghanistan


Waandishi wa habari wakiwa karibu na gari lililofyatuliwa risasi wakati wa shambulizi linaloendelea mjini Kabul. Septemba 13,2011

Waasi wa Taliban wanadai kuhusika na mashambulizi nchini Afghanistan katika ofisi za NATO

Waasi wa Taliban wanadai kuhusika kwa mifululizo ya mashambulizi yanayoendelea katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, Jumanne ambayo imelenga makao makuu ya jeshi la kimataifa la ushirika-NATO na majengo kadhaa ya serikali katika eneo. Ripoti za vyombo vya habari Marekani zinasema kuwa ubalozi wa Marekani Kabul pia ulishambuliwa.

Mfanyakazi wa Sauti ya Amerika pia amethibitisha kutokea milipuko isiyopungua miwili karibu na ubalozi wa Marekani.

Kumekuwepo na milipuko mfululizo pamoja na milio ya risasi karibu na makao makuu ya jeshi la msaada la ulinzi wa kimataifa huko Kabul.
Vyombo vya habari vinaripoti kwamba ghasia zipo kwenye eneo la kati la Kabul, karibu na eneo la kidiplomasia.

Taliban inasema inafanya shambulizi kubwa la kujitoa mhanga dhidi ya majengo ya serikali na idara za ujasusi nchini humo.
Hakuna ripoti za haraka kuhusu vifo.

Shambulizi hilo limetokea siku kadhaa baada ya waasi kufanya shambulizi moja kwenye kituo cha NATO kati kati ya Afghanistan, na kuwauwa raia wanne wa Afghanistan na kuwajeruhi zaidi ya watu 100 wengine wakiwemo wanajeshi 77 wa Marekani.

Taliban ilidai kuhusika kwa shambulizi la Jumamosi nje ya mlango mkuu wa Combat Outpost Sayed Abad katika jimbo la Wardak. Lakini msemaji wa Pentagon, George Little, alisema Jumatatu kuna hisia kali kwamba uongozi wa Haqqani wenye makao yake Pakistan ulisaidia na ulifahamu kuhusu shambulizi.

XS
SM
MD
LG