Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 02:44

Takriban wahamiaji 5,000 wanashikiliwa katika vituo rasmi vya vizuizi nchini Libya


IOM inawasaidia wahamiaji kutoka Libya
IOM inawasaidia wahamiaji kutoka Libya

Takriban wahamiaji 5,000 wanashikiliwa katika vituo rasmi vya vizuizi nchini Libya na wanawakilisha kiwango kidogo tu cha hali halisi mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji -IOM alisema Jumatano. 

Inasalia kuwa jambo lisilokubalika hata kidogo katika suala la ukiukwaji wa haki za wahamiaji nchini humo. Daima tumekuwa tukiweka wazi kwamba kuwekwa kizuizini sio suluhisho mkurugenzi mkuu wa IOM Antonio Vitorino alisema wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa mjini Geneva. .

Chini ya Umoja wa Mataifa, IOM inashirikiana na shirika la wakimbizi la UNHCR kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa wahamiaji katika vituo rasmi vya kizuizi.

Lakini tunaogopa kwamba kuna vituo visivyo rasmi vya kuwaweka watu kizuizini ambavyo hakuna wakala wowote mwenye aina yoyote ya taarifa na ufahamu Vitorino alisema.

Libya imekuwa njia inayopendelewa zaidi kwa maelfu ya wahamiaji kutoka Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Mashariki ya Kati na Asia Kusini wanaotaka kufika Ulaya baada ya kuanguka kwa utawala wa Moamar Gadhafi mwaka 2011.

Wakati wahamiaji wanaokhatarisha maisha yao katika Bahari ya Mediterania wanazuiliwa na mamlaka, wengine wanarudishwa kwenye pwani ya Libya na kuwekwa katika vituo vya kizuizi. Wanashutumiwa mara kwa mara na Umoja wa Mataifa kwa hali zao duni

XS
SM
MD
LG