Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 07:55

Tajiri anayetarajiwa kuimiliki kampuni ya Twitter yuko tayari kumruhusu Donald Trump kutumia tena mtandao huo


Picha inayomtambulisha Elon Musk yaonekana kwenye nembo ya Twitter, April 28, 2022. Picha ya Reuters
Picha inayomtambulisha Elon Musk yaonekana kwenye nembo ya Twitter, April 28, 2022. Picha ya Reuters

Tajiri anayetarajiwa kuwa mmiliki wa kampuni ya Twitter Jumanne amesema atamuruhusu rais wa zamani wa Marekani Donald Trump kutumia tena akaunti yake ya Twitter.

Musk ambaye anapanga kuinunua Twitter kwa kitita cha dola bilioni 44 amesema “ Sidhani kwamba haikuwa sahihi kumpiga marufuku Trump.”

“Nadhani ilikuwa kosa kwa sababu ilitenganisha sehemu kubwa ya nchi na hatimae hatua hiyo haikupelekea Donald Trump kutopata nafasi ya kujieleza.”

Akaunti ya Trump ilipigwa marufuku kabisa baada ya ghasia za January 6 kwenye bunge la Marekani, huku Twitter ikisema Trump kuendelea kutumia jukwa hilo ni hatari ya kuchochea ghasia nyingine.

“Uhuru wa kujieleza ndio msingi wa demokrasia ya ukweli, Twitter ni uwanja mpana wa kidijitali ambapo mambo muhimu kwa mstakabali wa binadamu yanajadiliwa,” Musk alisema katika taarifa ya hivi karibuni.

Trump alisema hana nia ya kujiunga tena na Twitter na atajikita zaidi kwenye mtandao wake aliouanzisha unaoitwa Truth Social.

XS
SM
MD
LG