Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 09:28

China yaahidi kushirikiana na utawala wa Trump


Waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi
Waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi

Waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi aahidi kuwa nchi yake itaendelea kujitahidi kuboresha uhusiano wake na Marekani.

Waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi alielezea wasiwasi wake kuwa mahusiano na Marekani yanaweza kuona mkanganyiko mpya na njia pekee ya kuendeleza mahusiano thabiti ni kwa kuheshimiana katika “maslahi ya msingi.”

Matamshi ya waziri Wang Yi yalionyesha kusisitiza kuwa msimamo wa China juu ya Taiwan hauna mashauriano, wiki kadhaa baada ya rais-mteule Donald Trump kupendekeza kwamba huenda akaifanyia tathmini sera ya Marekani kuhusu hadhi ya Taiwan.


Wang ameliambia gazeti la “People’s Daily” ambalo ni sauti ya Chama cha kikomunisti kuwa ataendelea kujitahidi kuboresha ushirikiano na Marekani lakini tayari ameona “kuna viashiria vipya na vya kukanganya na hali ya kutokuwa na uhakika ambayo inaathiri mahusiano yao, chini ya utawala wa wa Trump.

China imelalamika baada ya Trump mwezi huu kuhoji sera ya Marekani ambayo tangu mwaka 1979 imeitambua Beijng kama serikali ya China na ilikuwa inaendeleza mahusiano yasiyo rasmi na Taiwan.

Maoni ya rais-mteule juu ya Taiwan, ukichanganya na tuhuma kwamba China inachakachua sarafu yake na vitisho vyake vya kuanzisha kodi za juu dhidi ya bidhaa zinazoingizwa kutoka China, zimetikisa mahusiano kati umataifa haya mawili yenye uchumi mkubwa duniani.

Timu ya mpito ya Trump ilitangaza Jumatano kwamba Peter Navarro, mchumi ambaye ni mhadhiri wa Chuo kikuu cha California, ambae aliyeishutumu China kwa makusudi kabisa kuanzisha vita vya kiuchumi dhidi ya Marekani, kuwa sasa ataongoza baraza la sera ya biashara katika Ikulu ya Marekani.

Licha ya hilo, bado mahusiano ya Marekani na China kwa ujumla yanaelekea katika ushirikiano thabiti na wenye manufaa kwa wote, Wang amesema. Amekatiti usemi maarufu wa kichini ambayo uliwahi kutumiwa na rais Xi Jinping akitolea mfano wa mto ambao unatiririka bila ya kipingamizi, pasi na kuzuiliwa na vikwazo vilivyopo mlimani.

XS
SM
MD
LG