Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 14:52

Taharuki yatanda Bungoma baada ya mtu mmoja kuuawa


Maafisa wa polisi warusha vitoa machozi kwa waandamanaji Kenya.
Maafisa wa polisi warusha vitoa machozi kwa waandamanaji Kenya.

Maeneo kadhaa ya mji wa Bungoma yalishuhudia makabiliano makali kati ya polisi na waandamanaji Ijumaa asubuhi kufuatia kuuawa kwa mkazi mmoja. Waandamanaji waliwaambia waandishi wa habari kwamba mtu huyo aliuawa na polisi katika mtaa wa Muteremuko Eastate.

Moshi ulitanda baada ya vitoa machozi kurushwa na polisi wakikabiliana na wakazi waliojawa na ghadhabu.

Mkazi wa mji huo, Kaluna Asika, aliiiambia Sauti ya Amerika kwamba alishuhudia polisi wakimtoa mtu huyo kwa nyumba yake na kumpiga risasi.

Waandamanaji katika mji huo wa Magharibi mwa Kenya wamekuwa wakipinga uchaguzi uliofanyika siku ya Alhamisi wakishirikiana na wenzao katika maeneo mbali mbali yaliyo ngome ya upinzani.

Hata hivyo, Sauti ya Amerika imejaribu kupata kauli ya inspekta mkuu wa polisi bila mafanikio.

Makabiliano kati ya waandamanaji katika kaunti ya Migori yalikuwa yakiendelea wakati wa uchapishaji wa ripoti hii.

Idhaa hii inafuatilia habari hizi kwa karibu.

Wakati huo huo, wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo ya uwakilishi bunge walianza kuwasili katika kituo cha kitaifa cha kujumulisha kura cha Bomas of Kenya Ijumaa asubuhi.

Wasimamizi hao maarufu kama Returning Officers wanatarajiwa kuwasilisha fomu zote za 34A na 34B kabla ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.

Kufikia saa kumi na mbili asubuhi, idadi ya wapiga kura waliojitokeza ilikuwa imeripotiwa kama 33.4% (6,553,858) katika maeneo bunge 267. Hayo ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati.

Waandamaji wa upinzani Kenya.
Waandamaji wa upinzani Kenya.

Alhamisi jioni, Chebukati alitangaza kwamba uchaguzi utarudiwa Jumamosi kwenye majimbo manne ya Kisumu, Siaya, Migori na Homa Bay, pamoja na maeneo mengine ambayo uchaguzi ulivurugika Alhamisi kufuatia makabiliano kati ya walinda usalama na wafuasi wa upinzani.

Hata hivyo, gavana wa Kisumu, Anyang' Nyong'o amesema kuwa wakazi wa kaunti hiyo hawatashiriki.

-Na BMJ Muriithi

XS
SM
MD
LG