Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 17:04

Taasisi ya haki za binadamu (THRD) yalaani kukamatwa kiongozi wao


Gari la polisi likisubiri askari wakati walipokuwa wakimkamata Onesmo Ngurumwa Dar es Salaam
Gari la polisi likisubiri askari wakati walipokuwa wakimkamata Onesmo Ngurumwa Dar es Salaam

Mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu (THRD) nchini Tanzania, wamelaani vikali kitendo cha kukamatwa kwa mratibu wa kitaifa wa mtandao huo Onesmo Ole Ngurumwa.

Tamko hilo limetolewa leo jumamosi na mwanasheria wa THDR, Deogratius Bwire baada ya kukamatwa kwa mratibu huyo katika hoteli ya Blue Pearl saa tatu asubuhi.

Kitendo hicho kimetokea wakati viongozi hao wakiwa wanajiandaa kuingia kwenye uzinduzi wa kitabu cha 'sauti ya watetezi wa haki vyuoni '.

Bwire amesema mpaka sasa hakuna taarifa rasmi za kukamatwa kwao baada ya wakili Jones Semdodo aliyoko kituo cha polisi cha magomeni kusema hakuna makosa yaliyoainishwa na wanasubiri maelezo kutoka juu.

Amesema serikali na vyombo vya dola zifanye shughuli zao kihalali pasi na kuonea watu ambao wanafanya shughuli zao kihalali.

Lakini baadhi ya vyanzo vya habari vimesema tayari kiongozi huyo ameachiwa kwa dhamana.

XS
SM
MD
LG