Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 10:16

Mji wa kale wa Syria, Palmyra wakombolewa


Mji wa kale wa Palmyra nchini Syria

Wanajeshi wa serikali ya Syria wakisaidiwa na mashambulizi ya anga kutoka ndege za kijeshi za Russia, wameuteka tena mji wa kale wa kihistoria wa Palmyra kutoka wapiganaji wa Islamic State. Mashahidi hata hivyo wanaripoti kutokea kwa mashambulizi ya hapa na pale ndani ya mji amba ulikuwa umetekwa na wanamgambo wa Ilamic State takriban mizi 10 ilopita.

Msemaji wa jeshi la Syria alidai ushindi wa wanajeshi wa serikali kwenye televisheni ya taifa.

Alisema vikosi vya jeshi la Syria vikisaidiwa na ndege za kivita za Russia vimefanikiwa kurejesha amani na usalama kwa mji wa Palmyra na maeneo ya karibu, kufwatia operesheni kubwa zilofanywa, na kusababisha kuuliwa kwa wapiganaji wengi wa Islamic state na kuharibu silaha zao.

Rais Vladimir Putin wa Russia, amempongeza rais wa Syria Bashar al Assad kwa kuuteka tena mji huo wa kale akisisitiza umuhimu wa kuhifadhi makumbusho ya dunia kama ilivyotangazwa na UNESCO.

Kwa upande mwengine Rami Abdel Rahman, anaeonngoza kundi la kutetea haki za binadam la Syrian Observatory for Human Rights aliviambia vyombo vya habari vya kiarabu kuwa anaamini kundi la Islamic State bado linadhibiti baadhi ya sehemu katika mji huo.

Bw Abdel Rahman alisema, idadi kadhaa ya wajitowa mhanga wa Islamic State bado wapo ndani ya mji. Milio ya bunduki ilisikika katika baadhi ya wilaya na mapigano yalikuwa yakifanyika katika uwanja wa ndege wa kijeshi uliyo karibu na mji huo.

Abdel Rahman anadai kuwa ndege za kivita za Russia zimefanya takriban mashambulizi elfu moja ya anga katika juhudi za kutorosha wapiganaji wa Islamic State kutoka Palmyra.

Mchambuzi wa masuala ya kijeshi wa Syria Turki Saqr, aliambia televisheni ya taifa kuwa ushindi wa serikali dhidi ya Islamic State huko Palmyra, sasa unafunguwa njia kwa msukumo wa mwisho dhidi ya kundi la kigaidi katika mji wa jangwani wa Deir Ezzor, karibu na mpaka na Iraq.

XS
SM
MD
LG