Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 09:33

Syria na Russia walaumiwa kufanya kampeni za mabomu Aleppo


Wafanyakazi wa kutoa msaada wakiwasaidia majeruhi huko Aleppo, Syria.
Wafanyakazi wa kutoa msaada wakiwasaidia majeruhi huko Aleppo, Syria.

Wafanyakazi wa kutoa msaada katika mji wa Aleppo uliokumbwa na misukosuko nchini Syria wanasema Syria na mshirika wake Russia siku ya jumatatu waliongeza kampeni zao za mabomu kwenye maeneo ya mashariki mwa mji yaliyoshikiliwa na waasi nchini humo na kuuwa watu wasiopungua 100 katika siku ya nne mfululizo.

Wafanyakazi wa kutoa msaada kutoka jamii ya wamishionari wa kianglikana wameandika kwenye mtandao wa “twitter” wakisema vifo vinajumuisha watoto. Pia walisema wafanyakazi wa huduma za kutoa madawa na wa mahospitali wamechoshwa huku kukiwa hakuna vifaa vya ziada vinavyowasili.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, akijibu ripoti hiyo alisema serikali ya Syria ya Rais Bashar al-Assad na washirika wake Russia, “wanaonekana kuwa na nia ya kuuteka mji wa Aleppo na kuuharibu wakiwa katika utaratibu wa kuuteka.

XS
SM
MD
LG