Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:42

Kusitishwa mapigano Syria kunaleta matumaini


Mtoto raia wa Syria akiondolewa kutoka mji ulokumbwa na vita wa Aleppo.
Mtoto raia wa Syria akiondolewa kutoka mji ulokumbwa na vita wa Aleppo.

ankara inaweza kuwadhibiti wapiganaji wa kambi ya upinzani ambao wanakiuka sitisho la mapigano, kwani wana uwezo wa kuzuia silaha ambazo zinapitia katika nchi yao.

Kusitishwa kwa vita nchini Syria kunaonyesha matumaini tokea Ijumaa nchini humo, lakini mapambano karibu na mji wa Damascus na mashambulizi ya ndege za serikali katika maeneo ya wapinzani katika jimbo lla kaskazini Hama kunathibitish udhaifu uliopo katika juhudi za kutafuta amani.
Waangalizi kutoka Uingereza wanaofuatilia masuala ya haki za binadamu Syria wametoa taarifa kuwa ndege za kivita za serikali ya Syria zilifanya mashambulizi yasiyo pungua 16 dhidi ya wapinzani katika jimbo la Hama Ijumaa. Mkuu wa waangalizi hao Rami Abdel Rahmen amesema haikuwa bayana nani aliyeanza mapambano hayo.

“Mapambano yalizuka na yanaendelea… wakati helikopta zikishambulia sehemu zinazokaliwa na wapinzani na la Fateh al-Sham Front,” alisema, kama ilivyo ripotiwa na Shirika la habari la Ufaransa, akiongeza kuwa mapambano hayo yalikuwa ni ukiukaji wa makubaliano ya amani, lakini haikuwa wazi ni upande gani ulihusika katika kuanzisha hilo.

Fateh al-Sham Front, inayo julikana siku za nyuma kama Al-Nusra Front, ni mshirika wa zamani wa al-Qaida, kundi ambalo serikali ya Syria imesema lilitengwa kwenye mazungumzo ya usitishaji vita uliokubaliwa na Uturuki na Russia.
Lakini kundi la wapinzani limesema linaelewa kuwa kusimamishwa kwa mapambano ni kwa eneo lote ya Syria. Upinzani wa Syrian National Coalition, ambao unaungwa mkono na nchi za magharibi na baadhi ya mataifa ya ghuba umesema utaheshimu sitisho la mapigano lakini umeonya utajibu mashambulizi yote yatakayokaidi makubaliano ya kusitisha mapigano.

Waangalizi wa haki za binadamu hawakutangaza kuwepo majeruhi au vifo vyovyote tangu usitishaji mapigano ulipoanza Ijumaa.

Lakini mengi bado yanatatizo kuelewa kuhusu usitishaji huo wa vita nchini Syria ambao Rais wa Russia, Vladimir Putin alitangaza Alhamisi --makubaliano ya kusitisha mapambano ambayo Moscow imesema inaweza kufungua njia kwa mazungumzo yanayosimamiwa na Russia katika kutafuta suluhisho la vita vilivyodumu kwa takriban miaka mitano.

Lakini ushirika wa Uturuki katika mazungumzo haya umeongeza umuhimu, amesema mwanadiplomasia wa Magharibi, ambaye ametengwa katika suala hili.

Ankara inaweza kufanya mengi kuwadhibiti wapiganaji wa kambi ya upinzani ambao wanavunja makubaliano ya kusitisha mapigano, kwani wana uwezo wa kuzuia silaha ambazo zinapitia katika nchi yao.

XS
SM
MD
LG