Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 22:46

Suu Kyi: Demokrasia ni kustahmilia maoni ya wengine


Kiongozi wa kutetea demokrasia Burma Aung San Suu Kyi akibeba bango inayoeleza kwamba "mimi pia ninawapenda wananchi" siku moja baada ya kuachiliwa huru.
Kiongozi wa kutetea demokrasia Burma Aung San Suu Kyi akibeba bango inayoeleza kwamba "mimi pia ninawapenda wananchi" siku moja baada ya kuachiliwa huru.

Akizungumza katika siku yake ya kwanza tangu kua huru, kiongozi wa upinzani wa Burma Aung San Suu Kyi, ametoa wito wa kuwepo na mazungumzo ya moja kwa moja kati ya serikali ya kijeshi na upinzani.

Bila ya kupoteza wakati baada ya kufunguliwa kutoka kifungo cha karibu miaka 15, mshindi wa tunzo la Amani la Nobel, aliwahutubia wafuasi wake siku ya Jumapili, nje ya makao makuu ya chama chake cha National League for Democracy, akisema, "ninafahamu kile wananchi wanachokitaka" Maelfu ya wafusi wake katika mji mkuu wa Rangoon walijibu naye, "ni demokrasia."

Bila ya kua na uwoga, Bi Suu Kyi alizungumzia uchaguzi wa wiki ilyiopita akisema , ni lazima kwa uchaguzi ufanyike kwa njia iliyo sawa, na uchaguzi usio wa haki hautaleta demokrasia. Alisema "demokrasia haimanishi kwamba kila mtu anakubaliana na mwengine, bali ina maana kwamba inabidi kustahmilia maoni ya wengine."

Akizungumza na Sauti ya Amerika mtetea mkuu wa demokrasia huko Burma, alitoa wito kwa Jumuia ya Kiamtaifa kuwasiadia kupatikana mageuzi ya kweli nchini mwake.

Viongozi wa kila pemba ya dunia walipongeza kuachiliwa huru wa Bi Suu Kyi, huku wakitoa wito wakuachiliwa huru wafungwa wengine wa kisiasa wanaoshikliwa nchini humo na kwengineko.

XS
SM
MD
LG