Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 19:14

Sugu, Masonga wa Chadema waachiwa baada ya siku 24


Mbunge Joseph Mbilinyi (Sugu)

Mahakama ya Hakimu Mkazi-Mbeya imewaachia kwa dhamana washtakiwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Tanzania, Joseph Mbilinyi (Sugu) na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga baada ya kukaa mahabusu kwa siku 24.

Vyanzo vya habari vimefafanua Jumapili kuwa Sugu na Masonga walinyimwa dhamana kwa muda wote huo na mahakama hiyo kutokana na hoja za upande wa Jamhuri ukidai kuwa wanahofia usalama wao na kuwa shauri lake litasikilizwa kwa haraka na kuisha haraka.

Kesi inayowakabili ni ya madai kuwa walitumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite amewaachia kwa dhamana wawili hao baada ya Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala kuiambia mahakama hiyo kwamba imeshafunga ushahidi wake ambapo mashahidi sita walitoa ushahidi wao.

Mawakili wa pande zote mbili walikubaliana kwamba Februari 19 watawasilisha majumuisho ya shauri hilo mahakamani hapo.

Hakimu Mteite amekubaliana na hoja hiyo ya mawakili na kusema hukumu ya kesi hiyo itatolewa Februari26 mwaka huu.

"Washtakiwa wote wanaachiwa kwa dhamana, na kila mmoja atajidhamini mwenyewe kwa hati ya dhamana ya maneno ya Sh5 milioni kwa kila mmoja.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG