Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 10:08

Msanii wa Sudan Kusini atumia mziki kama mbinu ya kutetea maslahi ya umma


Raia wa Sudan kusini
Raia wa Sudan kusini

Nchini Sudan kusini, muimbaji wa mtindo wa rap Lual D’awol anatumia muziki wake kuzungumza dhidi ya serikali na ina sifa ya kunyamazisha sauti za wapinzani.

Kwa muimbaji wa rap wa Sudan kusini, Lual D’awol, mziki unaweza kuwa kitendo cha ukaidi wa kisiasa.

Alipanda jukwaani kwenye klabu moja yausiku mjini juba baada ya wanajeshi kuvamia sehemu nyingine kusitisha maonyesho yake. Katika tukio jingine mashabiki wake walimtowa kwa mlango wa nyuma ili kuzuia kukamatwa kwake.

Lual anasema, hip hop ni aina ya mziki ambao unaweza kuzungumza. Unatuma ujumbe na kuzungumza kuhusu madhila ya watu, na kuwa sauti ya wale wasokuwa na sauti. Na nahisi Sudan kusini kuna watu wengi wasio na sauti, kuna dhulma nyingi ns hakuna haki.

Lual ni mmoja wapo wa waimbaji mashuhuri wa rap Sudan Kusini. Alikulia Marekani, Lual alirejea nyumbani mwaka 2009 wakati huo likiwa ni eneo la kusini mwa sudan kwa matarijio ya kuisaidia nchi yake kukua.

Sudan Kusini ilipata uhuru wake miaka 2 baadae, lakini tangu wakati huo imeshuhudia vita, umasikini na rushwa.

Mashairi ya Lual yanasukuma vikwazo vya uhuru wa kuzungumza katika taifa ambalo watu ambao ni wakosoaji wa serikali wamefungwa, kupigwa n ahata kuuwawa.

Serikali imepiga marufuku kucheza kwenye vituo vya radio moja ya nyimbo maarufu za Lual inayouitwa “Dowla Jadit”.

“Dowla Jadit” inamaanisha taifa jipya kwa lugha ya kiarabu. Ndani ya wimbo huo, Lual anawakosoa maafisa wa ndani ambao anasema daima hujuibu kuwa sisi ni taifa jipya, kama kisingizio cha ukosefu wa huduma za umma kama vile maji na umeme. Lual anasema alipokea vitisho vya kifo baada ya kutoa kibao hicho.

Lual anasema, ni watu tu wanajaribu kunitia wasi wasi, na kunitisha na kujaribu kunifanya mimi niimbe nyimbo ambazo hazina maana au kuzungumzia mambo ya uwongo ambayo hata hayatokei, kama vile mambao ya kwenda klabu na kadhalika lakini hayo sio ukweli wa Sudan kusini.

Lual anasema hatakubali kunyanyaswa.

Anafanya kazi kuandaa album mpya, kwa kushirikiana na ma produza na waimbaji kutoka makabila tofauti ya nchini humo

XS
SM
MD
LG