Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 09:36

Sudan yashindwa kutia saini makubaliano ya demokrasia


Viongozi wa Sudan wameahirisha kutiwa saini kwa makubaliano yaliyopangwa kufanyika Jumamosi ili kurejesha kipindi kifupi cha mpito cha kidemokrasia, afisa mmoja amesema, huku hali ya kutoelewana ikiendelea kati ya makundi ya kijeshi.

Mapinduzi ya Oktoba 2021 yaliyoongozwa na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan yalivuruga mchakato ulioanza baada ya kuondolewa madarakani rais wa zamani Omar al-Bashir mwaka 2019.

Mkutano mpya kati ya makundi ya kijeshi na ya kiraia umepangwa kufanyika baadaye Jumamosi, alisema Khaled Omar Youssef, afisa wa kiraia aliyeondolewa madarakani na kukamatwa wakati wa mapinduzi ya Burhan ambaye sasa anahudumu kama msemaji wa mazungumzo hayo.

Wawakilishi kwa wiki kadhaa wamekuwa wakijadili sehemu ya mwisho ya mchakato wa kisiasa wa awamu mbili uliozinduliwa mwezi Disemba kwa masharti ya kurejesha utawala unaoongozwa na raia na uchaguzi wa kidemokrasia.

XS
SM
MD
LG