Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 11:13

Sudan yapiga mabomu vinu vya mafuta Sudan Kusini


Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir wakati wa mahojiano na televisheni ya taifa ya nchi hiyo akizungumzia mzozo wa nchi hizo mbili juu ya mafuta.
Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir wakati wa mahojiano na televisheni ya taifa ya nchi hiyo akizungumzia mzozo wa nchi hizo mbili juu ya mafuta.

Marekani yalaani Sudan kufanya mashambulizi maeneo ya raia huko Sudan Kusini.

Marekani imelaani vikali shambulizi la anga dhidi ya Sudan Kusini kwenye vinu vya mafuta yaliyofanywa na jirani zao Sudan. Katika taarifa Alhamisi msemaji wa wizara ya mambo ya nje Victoria Nuland alisema mashambulizi kama hayo kwa maeneo ya raia ni mabaya. Amesema Marekani inaitaka serikali ya Sudan kuacha mashambulizi ya anga ambayo anasema yanavunja sheria ya kimataifa. Msemaji wa jeshi la Sudan Sawarmi Khaled Saad amekanusha kuwa nchi yake ilihusika na mashambulizi hayo ya mabomu.

XS
SM
MD
LG