Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 15:17

Sudan yalaumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu

Rais wa Sudan , Omar Al Bashir kulia katika picha
Rais wa Sudan , Omar Al Bashir kulia katika picha

Mwenyekiti msaidizi wa chama tawala cha Rais Omar bashir cha National Congress, anasema shutuma zilizotolewa na kundi la Amnesty International zilikuwa na nia ya kudidimiza nchi ya Sudan.

Serikali ya Sudan inakanusha shutuma zilizotolewa na kundi moja la haki za binadamu kwamba nchi hiyo ilitumia silaha za kemikali katika mkoa wa Darfur.

Mwenyekiti msaidizi wa chama tawala cha Rais Omar bashir cha National Congress, anasema shutuma zilizotolewa na kundi la Amnesty International zilikuwa na nia ya kudidimiza nchi ya Sudan.

Mwenyekiti huyo msaidizi, Mahmoud Hamid amewaambia waandishi wa habari mjini Khartoum Alhamis kwamba shutuma za ukiukaji wa haki za binadamu zimekuwa zikitumiwa miaka ya nyuma, kama sababu ambayo haina ukweli wowote ili kuishambulia Sudan.

Wiki iliyopita, Amnesty ililishutumu jeshi la Sudan kwa kutumia silaha za kemikali dhidi ya raia, wakiwemo watoto katika mkoa wa Darfur katika muda wa miezi minane iliyopita.

Kundi hilo lenye makao yake Uingereza, lilisema lilikusanya ushahidi wa kutosha ikiwemo kupitia picha za satelaiti, na kufanya mahojiano ya kina na zaidi ya watu 200 walionusurika na kwamba wataalamu wamechambua darzeni ya picha katika uchunguzi wao.

XS
SM
MD
LG