Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 23:42

Sudan yaadhimisha miaka 67 ya Uhuru wake

Waandamanaji wa Sudan wakiandamana Khartoum, Sudan, Jumatatu, Desemba 26, 2022.AP
Waandamanaji wa Sudan wakiandamana Khartoum, Sudan, Jumatatu, Desemba 26, 2022.AP

Sudan imeadhimisha kumbukumbu ya miaka 67 ya Uhuru wake Jumapili  huku Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akiwapongeza watu wa Sudan katika siku hii kwa niaba ya serikali ya Marekani.

Sudan imeadhimisha kumbukumbu ya miaka 67 ya Uhuru wake Jumapili huku Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akiwapongeza watu wa Sudan katika siku hii kwa niaba ya serikali ya Marekani.

Amesema “ninavutiwa na ujasiri wa Wasudan ambao mara kwa mara walitaka sauti zao zisikike na kwamba viongozi wao watoe uhuru, amani na haki.Ninaungana na watu wa Sudan katika kuomboleza kupoteza maisha mwaka huu uliopita sio tu katika maandamano ya kuunga mkono demokrasia, lakini pia vurugu kati ya jumuiya”.

Aliongeza kusema kwamba anakaribisha tangazo la Desemba 5 la vyama vya Sudan kuhusu mfumo wa makubaliano ya kisiasa. Hii ni hatua muhimu ya kwanza kuelekea kurejesha mageuzi ya kidemokrasia ya Sudan. Marekani inathibitisha tena uungaji mkono wake kwa mchakato huu unaoongozwa na Sudan na inazisihi pande zote kushiriki haraka kwa nia njema na mazungumzo ya maana ili kutatua masuala ambayo hayajashughulikiwa alieleza.

Amesisitiza kwamba Marekani itaendelea kusimama pamoja na watu wa Sudan na mapambano yao ya demokrasia. Akitabanaisha kwamba anatazamia kuendelea kufanya kazi na Sudan wakati wa mabadiliko ya kidemokrasia na kuwatakia mwaka wenye amani na mafanikio.

XS
SM
MD
LG