Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 13:09

Sudan: Wanajeshi warusha gesi ya kutoa machozi hospitalini


Waandamanaji wanaopinga utawala wa kijeshi Sudan. Picha: AP
Waandamanaji wanaopinga utawala wa kijeshi Sudan. Picha: AP

Kijana mwenye umri wa miaka 19, ameuawa kwa kupigwa risasi katika maandamano ya hivi punde ya kupinga mapinduzi ya kijeshi ya mwaka uliopita nchini Sudan.

Madaktari wamethibitisha mauaji hayo.

Polisi walikabiliana na waandamanaji katika mji mkuu wa Khartoum na kurusha gesi ya kutoa machozi ndani ya hospitali walimokuwa wagonjwa.

Waandamanaji 94 wameuawa tangu kutokea mapinduzi ya kijeshi nchini Sudan, mwezi Oktoba.

XS
SM
MD
LG