Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 07:33

Sudan: Viongozi wa kijeshi na kiraia wafikia makubaliano ya kumaliza mzozo wa kisiasa


Kiongozi wa kijeshi wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan
Kiongozi wa kijeshi wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan

Viongozi wa kijeshi na kiraia wa Sudan leo Jumatatu wametia saini mkataba wa awali wenye lengo la kumaliza mzozo mkubwa wa kisiasa uliosababishwa na mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba mwaka jana.

Hatua hiyo imepelekea baadhi ya viongozi vyama vya upinzani kulalamika na kusema ni usaliti. Mkuu wa jeshi Abdel Fattah al Burhan alifanya mapinduzi Oktoba mwaka jana na kuvuruga kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Mgawanyiko mkubwa ulitokea miongoni mwa asasi za kiraia tangu mapinduzi hayo ambapo baadhi wakihimiza kuwepo na makubaliano na jeshi, wakati wengine wakisisitiza ya kutokuwepo na ushirikiano wala majadiliano na viongozi wa mapinduzi.

Makubaliano ya leo Jumatatu yalitiwa saini na mkuu wa kikosi cha wanamgambo cha Burhan , Mohamed Hamdan Dagalo na makundi kadhaa ya kiraia hasa mungano mkuu wa FFC.

Marekani na washirika wake Norway, Saudi Arabia Umoja wa Falme za kiarabu na Uingereza zimepongeza kutiwa saini makubaliano hayo.

XS
SM
MD
LG