Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:56

Mazungumzo juu ya Sudan bado kitendawili


Wawakilishi kutoka Sudan kaskazini na kusini katika mazungumzo yanayofanyika Addis Ababa, nchini Ethiopia juu ya hali ya mkoa wa Abyei unaogombaniwa nchini Sudan
Wawakilishi kutoka Sudan kaskazini na kusini katika mazungumzo yanayofanyika Addis Ababa, nchini Ethiopia juu ya hali ya mkoa wa Abyei unaogombaniwa nchini Sudan

Mazungumzo juu ya Sudan kaskazini na kusini juu ya hali ya mkoa wa Abyei unaogombaniwa bado yamekwama kwa zaidi ya wiki moja baafa ya viongozi kutangaza walikuwa karibu kufikia makubaliano.

Mazungumzo yataendelea Jumatatu mjini Addis Ababa huku Sudan kaskazini na kusini wakijaribu kusuluhisha masuala yaliyopo kabla ya Julai 9, tarehe iliyopangwa Sudan kugawanyika na kuwa mataifa mawili. Lakini wakati mashauriano yamezorota, khofu ya kurudi kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe inaongezeka.
Wiki moja iliy
opita Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir na kiongozi wa kusini Salva Kiir, walikubaliana kimsingi kuondoa majeshi yao katika mkoa wa Abyei wenye utajiri wa mafuta na kuruhusu walinzi wa amani wa Ethiopia kuwepo katika eneo hilo. Mkataba huo ulitakiwa kutiwa saini kwenye sherehe za Jumamosi jioni.
Lakini
utiaji saini ulicheleweshwa na mazungumzo yaliendelea kukwama Jumapili, wakati wapatanishi walipozungumzia hali ya baadae ya mkoa huo kufuatia uhuru wa Kusini. Pande hizo zinasemekana kuwa na msimamo mkali kuhusu suala hili, na wapatanishi wameripotiwa kukatishwa tamaa kwasababu majaribio yao kutaka kufikia muafaka hayajafua dafu.

Sitisho la mapigano la saa 72 lililobuniwa ili kuruhusu usambazaji wa mahitaji muhimu kwa wananchi katika jimbo la Kordofan kusini pia lilitishiwa na kukwama kwa mazungumzo ya kidiplomasia.

Wakati huo huo picha za satalaiti juu ya mkoa huo zinaonyesha kuwa majeshi ya Sudan kaskazini yanadhibiti mji wa mpakani wa Kadugli na kwamba maelfu ya raia wanakimbia kuelekea hifadhi za muda karibu na kituo cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa.

XS
SM
MD
LG