Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 02, 2022 Local time: 15:20

Mapambano yazagaa Sudan Kusini na Sudan


Waziri wa habari wa Sudan Kusini, Barnaba Benjamin(R) na msemaji wa jeshi Philip Aguer, wakiongea na vyombo vya habari kuhusu mapigano ya karibuni kati ya majeshi ya Sudan na Sudan Kusini

Mapambano kati ya Sudan Kusini na Sudan yameongezeka zaidi ya wiki mbili zilizopita

Maafisa wa jeshi wanasema mapambano yamezagaa kwenye mpaka wa Sudan na Sudan Kusini, huku maafisa wa Sudan wakidai kuteka eneo moja linalokaliwa na Sudan Kusini.

Afisa mmoja wa jeshi nchini Sudan Kusini alisema mapambano makali yameongezeka kwenye mgogoro wa mpakani ambao ulianzia kabla Sudan Kusini ilipojitenga kutoka Sudan mwaka jana.

Mapigano kwenye mpaka wa Kaskazini na Kusini yamekuwa yakitokea mara kwa mara zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Msemaji wa jeshi la Kusini, Kanali Philip Aquer alisema Jumatatu kwamba ndege ya anga ya Sudan iliwauwa raia watano katika mashambulizi kwenye mji wenye mzozo wa Heglig.

Kituo cha habari cha Sudan pia kiliripoti Jumatatu kwamba jeshi la Sudan lilichukua udhibiti wa Mugum, ngome ya jeshi la Kusini katika jimbo la Blue Nile, ambalo lipo karibu na mpaka na Sudan Kusini.

Idara ya habari ya serikali imekariri chanzo kimoja kisicho rasmi cha kamanda wa kitengo cha nne akisema kitengo hicho kilishambulia Mugum Jumapili na kuwauwa waasi 25 na kuzuia kiwango kikubwa cha silaha na vifaa.

Majeshi kutoka Sudan Kusini wiki iliyopita yaliuteka mji wa Heglig ulio kwenye mpaka wa eneo lenye utajiri wa mafuta lililodaiwa na Sudan.

Aguel, afisa wa jeshi la Kusini alisema mashambulizi holela dhidi ya Heglig pia yaliwajeruhi vibaya watu tisa na kupiga visima vya mafuta. Pia alisema kwamba mji wa Bentiu katika jimbo la Unity nchini Sudan Kusini lilipigwa na kwamba mgogoro umesambaa kuelekea majimbo kadhaa ya Kusini yanayopakana na Sudan, ikiwemo Western Bahr el Ghazal.

“Kumekuwepo na mashambulizi ya mabomu yanayoendelea kufanywa na majeshi yenye silaha ya Sudan,” alisema Aquel. Majeshi yetu hivi sasa yapo kwenye tahadhari ya juu.”

Mapigano yalizuka katika eneo linalogombaniwa la Abyei mwezi Mei mwaka jana, miezi kadhaa kabla ya Sudan Kusini kujitangazia rasmi uhuru wake.

XS
SM
MD
LG