Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 19:17

Mashambulizi Sudan yaua zaidi ya watu 240


Salva Kiir Mayardit, Rais wa serikali ya Sudan Kusini, Feb 8, 2011 (file photo)

Maafisa huko kusini mwa Sudan wanasema mashambulizi yaliyofanywa na mwanamgambo mmoja muasi yamesababisha vifo vya watu wasiopungua 240 wiki iliyopita, zaidi ya mara mbili ya idadi ya vifo iliyotangazwa awali.

Maafisa wa chama tawala cha Sudan People’s Liberation Movement-SPLM, walisema Jumanne kuwa watu wengi ambao walikufa kwenye mashambulizi katika wilaya ya Fangak, kwenye jimbo la Jonglei walikuwa raia. Walisema vifo pia vilijumuisha wanajeshi wa serikali na waasi 30. Wapiganaji waasi wanaomtii afisa wa jeshi George Athor, walifanya mlolongo wa mashambulizi huko Jonglei, Jumatano na Alhamisi iliyopita.

Athor alianzisha uasi baada ya kushindwa kinyang’anyiro cha kiti cha gavana katika jimbo la Jonglei katika uchaguzi uliofanyika April mwaka jana. Kundi lake lilitia saini kusitisha mapigano mwezi januari, siku chache kabla ya kura ya maoni ya kihistoria ya Sudan Kusini.

Katibu mkuu wa SPLM, Pagan Amum, alirudia kutoa shutuma Jumanne kwamba Sudan kaskazini inawapatia fedha na silaha waasi huko Kusini. Serikali ya Sudan huko Khartoum inakanusha shutuma hizo.


XS
SM
MD
LG