Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 15:21

Sudan na Sudan Kusini hatarini kuingia vitani tena.


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akisalimiana na wananchi.

Salva Kiir akaidi wito wa Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa kuondoa majeshi Heglig na kupelekea hatari ya kuingia tena vitani.

Rais wa Sudan kusini amekataa kuondoa majeshi ambayo yameteka mji wa mpakani ulio na mzozo na Sudan wiki hii.

Akizungumza na bunge alhamisi Salva Kiir amesema hatatoa amri ya kujitoa kwa vikosi vya Sudan Kusini kutoka mji wa Heglig, licha ya wito wa Umoja wa Afrika na Umoja wa mataifa kufanya hivyo.

Alisema pia kuwa majeshi ya sudan kusini huenda yakaingia katika eneo lingine la mpakani lenye mgogoro, Abyei, kama umoja wa mataifa hautalazimisha sudan kujitoa katika eneo hilo.

Uhasama kati ya Sudan na Sudan Kusini wiki hii umepelekea wasiwasi kuwa nchi hizo zitaingia tena kwenye vita.

XS
SM
MD
LG